WAGOMBEA WAWILI SHINYANGA VIJIJINI WAJIONDOA UCHAGUZI CCM - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 1 October 2022

WAGOMBEA WAWILI SHINYANGA VIJIJINI WAJIONDOA UCHAGUZI CCM

 

Wagombea nafasi ya Mwenyekiti CCM wilaya ya Shinyanga vijijini, (wakwanza kushoto) ni Edward Ngelela, na (wapili kutoka kulia) ni Mwenzetu Mgeja, ambapo nafasi hiyo wanagombea wawili tu mara baada ya wagombea wengine wawili kujitoa.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHAMA cha Mapinduzi CCM leo kinaendelea na uchaguzi wa ndani ya Chama wakutafuta nafasi ya Mwenyekiti wa CCM ngazi ya wilaya, pamoja na Wajumbe ambao watawakilisha kwenye nafasi mbalimbali.

Uchaguzi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wenyewe unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa, ambapo wagombea watatu wana wania nafasi ya Uenyekiti, ambao ni Pendo John Sawa, Mokhe Warioba Nassor na Magile Anold Makombe.

CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini wenyewe wanafanyika uchaguzi katika uwanja wa michezo wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga na wanaowania nafasi ya Mwenyekiti CCM ni Edward Ngelela, na Mwenzetu Mgeja, huku wagombea wawili wakijitoa kuwania nafasi hiyo ambao ni Peter Gawiza na Anna Ng’wagi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na watu wenye ulemavu akipiga kura kwenye uchaguzi wa CCM.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga kura kwenye uchaguzi wa CCM.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakar Mukadam akipiga kura kwenye uchaguzi wa CCM.
Wajumbe wakipiga kura.
Wajumbe CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakipiga kura.
Wajumbe CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini wakipiga kura.
Wajumbe CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini wakipiga kura.
Wajumbe wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa kwenye uchaguzi.
Wajumbe wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa kwenye uchaguzi.
Wajumbe wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa kwenye uchaguzi.
Wajumbe wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa kwenye uchaguzi.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum (katikati) akiwa kwenye uchaguzi wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijni.
Wajumbe wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini wakiwa kwenye uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso