BAADA YA ZAECA KUTAKIWA KUJITATHIMINI MKURUGENZI MKUU AJIUZULU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 2 September 2022

BAADA YA ZAECA KUTAKIWA KUJITATHIMINI MKURUGENZI MKUU AJIUZULU

Siku tano baada ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi kuitaka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (Zaeca) kujitathmini, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, ACP Ahmed Khamis Makarani.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Septemba 2, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu-Zanzibar, Charles Hilary, Rais Mwinyi amekubali barua ya kujiuzuluya Makarani.


Taarifa hiyo imesema hatua hiyo inafuata maelekezo ya Rais Mwinyi kuitaka Zaeca kujitathmini, baada ya hivi karibuni kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)


Jumamosi ya Agosti 27, 2022, Rais Mwinyi alikabidhiwa ripoti na CAG, Dk Othman Abbas Ali Ikulu Mjini Zanzibar ikianika madudu na ubadhirifu wa fedha za umma.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Rais Mwinyi aliinyooshea kidole Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (Zaeca), kuwa haina msaada kwa Serikali.


Rais Mwinyi alisema kama mamlaka zinazohusika zingekuwa zinafanya kazi, isingekuwa kila mwaka yanarudiwa kutajwa mambo yale yale ya ubadhirifu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso