RAIS WA ZAMBIA MHE.HAKAINDE HICHILEMA NA MHE. RAIS SAMIA WAAHIDI KUREJESHA MAHUSIANO YA KISIASA YALIYOPOTEA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 2 August 2022

RAIS WA ZAMBIA MHE.HAKAINDE HICHILEMA NA MHE. RAIS SAMIA WAAHIDI KUREJESHA MAHUSIANO YA KISIASA YALIYOPOTEA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya siku moja nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati Nyimbo za Taifa (Tanzania na Zambia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kwenye mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na matarumbeta vilivyokuwa vikitoa burudani wakati wa mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam.

***********************************************************



Tanzania na Zambia zimekubaliana kurejesha uhusiano wao ambao miaka ya karibuni ulilegalega, huku viongozi wa mataifa hayo wakikubaliana kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kuwaunganisha watu.


Rais wa Zambia Haikendi Hichilema amefanya ziara nchini ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuingia madarakani ambapo alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.


Katika mazungumzo hayo wawili hao wamekubaliana mambo kadhaa ikiwamo kurudisha umoja na mshikamano wa mataifa hayo ambayo yalikuwa na ukaribu mkubwa wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza ya Serikali za nchi zote mbili.


Akizungumza hilo Rais Samia amesema Serikali yake na ile inayoongozwa na Hichilema wamekubaliana kurejesha uhusiano wa kihistoria ambao nchi hizo uliziunganisha.


“Tanzania na Zambia ni ndugu hapa katikati uhusiano wetu ni kama ulilegalega sasa tumekubaliana kurudisha udugu wetu ambao umeonekana kupotea. Tunarudisha kwa kuangalia uhusiano wa kisiasa, sisi kama viongozi wa nchi tuwaongoze watu wetu waelewane, washirikiane na kuwa ndugu kama ambavyo waasisi wetu waliona inafaa,”.


Suala hilo lilizungumziwa pia na Rais Hichilema aliyeeleza kuwa, “Tunatakiwa kuimarisha uhusiano ulioanzishwa na waasisi wetu, ujirani tulio nao hatuna sababu ya kutengana.


Mipaka ya kijiografia isiwe chanzo cha kutenganana uhusiano wetu ni wa asili ukienda Tunduma na Nakonda kuna mwingiliano mkubwa kati ya watanzania na wazambia. Kama tusipowatengeneza mazingira ya ushirikiano basi watadhuriana,”.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso