BASI LA TANZANITE LAPATA AJALI SINGIDA WATU WATANO WAFARIKI DUNIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 18 August 2022

BASI LA TANZANITE LAPATA AJALI SINGIDA WATU WATANO WAFARIKI DUNIA

 


Watu watano wamefariki dunia akiwemo Mtoto mdogo katika ajali ya gari la Kampuni ya Tanzanite lenye namba za usajili T 916 DNU, ajali imetokea katika Kijiji cha Mbwasa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stella Mukabiliwa amesema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea Jana majira ya saa 9:30 Alasiri ni mwendokasi wa dereva uliosababisha tairi kupasuka ambapo baada ya ajali dereva alitoroka.


“Katika ajali hiyo waliofariki ni Watu watano akiwemo Mtoto mdogo na majeruhi ni wanne”

CHANZO:MILLARD AYO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso