NYONGEZA YA MISHAHARA SIO KWA WATUMISHI WOTE-WAZIRI MKUU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 29 July 2022

NYONGEZA YA MISHAHARA SIO KWA WATUMISHI WOTE-WAZIRI MKUU



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema asilimia 23 ya nyongeza ya mishahara iliyotamkwa iliwalenga watumishi waliokuwa wanalipwa kima cha chini ambao ni kati ya asilimia 75 hadi 78 ya wafanyakazi wote.


Majaliwa ametoa ufafanuzi huo leo Ijumaa Julai 29, 2022 wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu nyongeza ya mishahara, siku chache baada ya watumishi kulalamikia nyongeza hiyo na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kupinga.


Miongoni mwa malalamiko ya watumishi, ni kiwango kidogo cha nyongeza ya mishahara hiyo, ambayo Majaliwa amesema si wafanyakazi wote walioongezewa kwa asilimia 23, bali ni wale waliokuwa wanalipwa kima cha chini.


“Inapotamkwa wanaonufaika si wote hadi wa mishahara mikubwa, wanaonufaika ni wale wa kada ya chini, ambao kwa tangazo la mwaka huu wanufaika ni asilimia 75 hadi 78 ya watumishi wote,” amesema.


Amefafanua kuwa asilimia za nyongeza ya mishahara inapungua kwa kadri ya ukubwa wa kiwango cha malipo anachopata mfanyakazi, akitolea mfano mawaziri wameongezewa asilimia 0.7.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso