UMOJA WAANZA UJENZI WA HOSTELI WANAFUNZI WANAOTOKA MBALI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 20 June 2022

UMOJA WAANZA UJENZI WA HOSTELI WANAFUNZI WANAOTOKA MBALI


UMOJA wa Maendeleo ya Kijiji cha Kikukwe(UMKI),kilichoki Kata ya Kanyigo,wilayani Missenyi,wameanza ujenzi wa hosteli kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali na shule ya sekindari Kikukwe yenye kidato cha kwanza hadi cha nne,ikiwa ni mojawapo kati ya shule mbili za kata,katani humo,nyingine ikiwa ni shule ya sekondari Kigarama.

Na Mutayoba Arbogast - Bukoba



Picha ya pamoja ya wanaKamati ya ujenzi wa hosteli baada ya kikao kubariki ujenzi huo.(wa kwanza toka kushoto mstari wa mbele ni Eliud Mujemula ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi,wa pili kutoka kushoto ni Afisa mtendaji wa kijiji Kikukwe, Amina Majid,wa sita kutoka kushoto ni mwenyekiti wa UMKI,Godfrey Mugini,wa nne kutoka kulia ni Mwenyekiti wa kijiji Kikukwe,Josephati Ikula)


UMKI,ambayo imesajiliwa Halmashauri ya wilaya,ilianzishwa  mwaka 2021,hasa na wazaliwa wa kijiji hicho waishio miji mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi ili kurudisha fadhila kijijini kwao katika kuimarisha elimu na mipango ya maendeleo kiuchumi.


Waliwahamasisha pia wanakijiji kujiunga na umoja huo.


Kwa kutambua matatizo yanayowakumba wanafunzi wanaotoka mbali na shule hiyo,hasa watoto wa kike,waliona kuna umuhimu mkubwa kujenga hosteli shuleni hapo,ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha elimu.


Ili kuwahi shuleni,wanafunzi wanatoka mbali hulazimika kudamka majira ya saa kumi na moja alfajiri huku baadhi wakipita nyika,vilima na vichaka,jambo linalohatarisha maisha yao,akini wakati mwingine wakizembea kwenda shule kutokana na umbali,na hivyo kuzorotesha maendeleo ya elimu


Kikao cha ujenzi cha Kamati kinachoundwa na baadhi ya wananchi  na viongozi kijiji Kikukwe wa  Kikukwe,Kamati maalum ya UMKI kutoka Dar es salam na baadhi ya wananchi na viongozi wa kijiji jirani cha Bugombe ambacho wanafunzi wake wanasima hapo kimefanyika leo shuleni hapo,na kubariki kuanza kwa ujenzi huo,ambapo shughuli hiyo imeanza rasmi  leo,kwa kuchimba msingi.


Kwa mujibu wa Katibu mtendaji wa UMKI Magreth Kyai,hosteli hiyo itagharimu  sh milioni 156,na sasa wanachi wamechangia fedha taslimu nguvu kazi na  vifaa vya ujenzi,ambavyo ni mawe na mchanga,vyote jumla ni zaidi ya sh milioni 23.


Amesema baada ya kukamiisha ujenzi wa msingi,anatarajia halmashauri ya wilaya ya Missenyi kuwaunga mkono katika ujenzi huo kwani imekuwa nstari wa mbele kuwapa ushirikiano walipiwasiisha ombi lao la kujenga hosteli,huku akiwaomba wananchi wa vijiji hivyo viwili,kuendejea kuchangia fedha,nguvu kazi na vifaa vya ujenzi ili kusiwepo na kukwama katika hatua yoyote ya ujenzi.


Mwenyekiti wa kijiji cha Kikukwe,Josephati  Ikula amewashukuru wanachi  wa vijiji hivyo viwili,n wdngine wa kata ya Kanyigo kwa kujitolea kwao katika kuhakikisha usalama na ulizi wa mtoto unapewa kipaumbele ili wanafunzi waweze kufikia ndoto zao.


Mwenyekiti wa UMKI,Godfrey Muginiamesema UMKI imejipanga kuhakikisha maendeleo ya kijijicha Kikukwe yanakuwa ya kupigiwa mfano,na kuwa wakati wa maneno umekwisha,sasa ni vitendo,huku Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi,Eliud Mujemula akisema  kama mambo yatakwenda namna yalivyopangwa,hosteli itakamilika kwa wakati na kuwataka wazazi na walezi  kujiandaa kwa mahitaji ya wanafunzi watakapoanza kulala shuleni.


Aidha UMKI inawahamasisha wananchi kuima parachichi aina ya Hass,ambapo tayari wana vitalu vya miche, na pia uimaji wa vanilla ili jamii ya kata hiyo ya Kanyigo ijikomboe kiuchumi.





Uchimbaji msingi


Baadhi ya majengo shule ya sekondari Kikukwe

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso