THRDC YAJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO YA MTANDAO KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MTANDAO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 11 May 2022

THRDC YAJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO YA MTANDAO KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MTANDAO


Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu –THRDC Nuru Maro akizungumza  na wanahabari jijini Dar es salaam katika katika ukumbi wa Kisenga uliokutanisha wadau wa mtandao huo. 


Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania-THRDC umesema utandelea kushirikiana na Serikali, katika kuhakikisha wanasaidia utetezi wa haki za binadamu kwa wananchi ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo kwani jamii inahitaji kuona haki inatendeka katika jamii.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu –THRDC Nuru Maro wakati akizungumza katika mkutano uliokutanisha wadau wa haki za binadamu nchini wakifanya tathmini ya miaka kumi ya Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu nchini THRDC kujadili changamoto na mafanikio ya mtandao huo katika kuitumikia jamii.

Amesema malengo yao ni kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na wadau wote wa watetezi wa haki za binadamu,ikiwa ni pamoja na serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ili kuweza kuwasaidia wananchi.

THRDC tumekuwa tukishirikiana na Mahakama zote Tanzania Bara na Zanzibar na hivi karibuni tunaingia makubalino na Mahakama ya Zanzibar baada ya kuona changamoto zinazokabili serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kuona changamoto ya masuala ya Kijinsia, haki za watoto kuvunjwa na baada ya kuona kazi kubwa inayofanywa na wanamtandao serikali ya mapinduzi ikakubalina na sisi tufanye kazi kwa pamoja’amesema Wakili Maro

Wakili Maro pia ameishauri Serikali kuridhia mkataba wa kimataifa wa watetezi wa haki za binadamu wa mwaka 1998 unaolenga kulinda usalama wa watetezi wa haki za binadamu nchini ili kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira salama ya kusaidia jamii.

Awali akizungumza Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kwa kanda ya Mashariki na Pwani na  Mkurugenzi wa Shirika la C-SEMA Michael Marwa amesema kwa tahmini waliofanya unaonyesha uhusiano unaendelea kuimarika baina ya Watetezi na Serikali tofauti na miaka ya nyuma.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kwa kanda ya Mashariki na Pwani na  Mkurugenzi wa Shirika la C-SEMA Michael Marwa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Equality Growth (EFG) na Mjumbe wa THRDC Jane Magigita amesema watetezi wanasimama kwa ajili ya kuwatetea watu na nchini Tanzania kumekuwa na ufanisi mkubwa katika masuala ya utetezi wa kulinda haki za kibinadamu.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania-THRDC
Mei 13 mwaka huu ambapo wanachama pamoja na wadau zaidi ya 300 watashiriki katika maadhimisho hayo yatakayofanyika jijini Dar es salaam.


Mratibu wa Mtandao Ndugu Onesmo Olengulumwa akiwa na wageni waalikwa wakati wa mdahalo juu ya watetezi wa haki za binadamu ukiangazia mafanikio na changamto kwa miaka 10 ya mtandao


Wanachama na wadau wa Mtandao waliohudhuria mdahalo juu ya watetezi wa wa haki za binadamu kuangazia miaka 10 ya mtandao kujadili mafanikio na changamoto kuelekea kilele cha maadhimisho yatakayofanyika jijini Dar es salaam

Baadhi ya wanachama wakiwa na meza kuu walioshiriki mdahalo juu ya watetezi wa wa haki za binadamu kuangazia miaka 10 ya mtandao kujadili mafanikio na changamoto 

Meza kuu pamoja na Waratibu wa kanda wa Mtandao wa THRDC wakiwa picha ya pamoja wakati wa mdahalo juu ya watetezi wa wa haki za binadamu kuangazia miaka 10 ya mtandao kujadili mafanikio na changamoto

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso