MWANAMKE WA KWANZA ATEULIWA KUWA MGOMBEA MWENZA URAIS - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 16 May 2022

MWANAMKE WA KWANZA ATEULIWA KUWA MGOMBEA MWENZA URAIS



Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amemteua Martha Karua kuwa mgombea mwenza wake, na kumfanya mwanasiasa huyo mkongwe kuwa mwanamke wa kwanza kuwania urais kwa tiketi ya chama kikuu cha siasa.


Bi Karua, aliyekuwa waziri wa sheria na mgombeaji urais, anatoka eneo la kati ambalo lina idadi kubwa zaidi ya wapiga kura waliosajiliwa nchini.


Akizungumza katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta, Bw Odinga alimsifu Bi Karua kwa bidii na rekodi yake ya haki za binadamu.


"Nilimhitaji Joshua wa kweli kwenye kando yangu, ambaye hatakuwa koti la ziada. Baada ya kutafuta na kutafakari, pamoja na mashauriano, nimefikia uamuzi kwamba anayeshikilia nafasi hii lazima awe mwanamke," Bw Odinga alisema.


Bw. Raila Aliongeza: "Ofisi ya Naibu wa Rais ni ofisi mbayo haiwezi kushindana na urais. Anayeshikilia wadhifa huo lazima awe mfanyakazi mwenza"


Iwapo atachaguliwa mwezi Agosti mwanasiasa huyo mkongwe atakuwa naibu wa rais wa kwanza mwanamke wa Kenya.


Mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa mgombea mwenza Bi Karua alisema: ''Huu ni wakati wa wanawake wa Kenya. Ni wakati ambao bibi yangu angejivunia...lakini sishangai kwa sababu vizazi vya wanawake vimepigania mabadiliko. Huu ni wakati wetu kama wanawake wa Kenya. Pia ni wakati kwa wanaume: ni ndugu na baba zetu.


Pia alichukua muda huo kuelezea safari yake ya kisiasa na kiongozi huyo wa Azimio akiongeza kuwa ana rekodi imara ya kutetea Wakenya na hivyo basi ndiye anayefaa zaidi kuwa rais.


Bi Karua, alijiunga na timu ya Azimio mnamo Machi amekuwa akizunguka nchi nzima akipigia debe uungwaji mkono kwa Bw Odinga.


Wiki iliyopita, alihudhuria mahojiano ya mgombea mwenza ambapo alisema atakubali uamuzi wa jopo la mahojiano.


Chaguo la Martha Karua limegawanyika Azimio ambayo ilimfanya kiongozi wa chama cha Wiper Kenya na makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka kujitenga na muungano huo.


Katika kikao tofauti na wanahabari, Bw Musyoka alimtakia Bi Karua kila la heri.


"Namtakia kheri mgombea mwenza wa Railas Martha Karua. Tumekubali kwenda njia tofauti. Nilimwambia Raila uamuzi wa kuchagua Karua utakabiliwa na upinzani mkubwa. OKA itapambana kivyake na hivi karibuni Wiper itazindua manifesto yake yenyewe," alisema.

CHANZO:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso