MLINZI ADAIWA KUUA MCHIMBAJI MADINI MWAKITOLYO AKIGOMBANA NA MKEWE MWAKITOLYO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 19 May 2022

MLINZI ADAIWA KUUA MCHIMBAJI MADINI MWAKITOLYO AKIGOMBANA NA MKEWE MWAKITOLYOKamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga George Kyando akizungumza na vyombo vya habari.Pikipiki ya Kamanda wa Sungusungu ikiwa imeteketezwa moto.

Ofisi ya Mwenyekiti wa kitogoji ikiwa imebomolewa


WANANCHI wa Kitongoji Namba 2 Kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wameichoma moto nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho Shabani Zoro, na kuvunja nyumba ya Kamanda wa Sugusungu Buyaga Kazimoto na kuharibu mali zao zingine ikiwamo Ofisi baada ya kushikwa na hasira kusababisha mauaji ya mwenzao Jackson Joseph aliyeuawa kwa kupigwa Risasi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, amebainisha hay oleo Mei 19, 2022 wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Amesema tukio la kuchomwa moto nyumba ya mwenyekiti huyo wa kitogoji Shabani Zoro, kuvunja Ofisi na duka lake pamoja na kuvunjwa nyumba ya Kamanda wa Sugusugu Buyaga Kazimoto na kuchoma moto pikipiki yake, limetokea baada wananchi kuutuhumu uongozi huo kukithiri kuonea wananchi na kusababisha kifo cha mwenzao.

Kyando anaeleza kuwa Mei 17 mwaka huu majira ya saa 5 usiku, marehemu Jackson Joseph (35) alikuwa na ugomvi na mkewake Ester Emmanuel (23) na baada ya ugomvi kuwa mkubwa Mwanamke alikimbilia kwa jirani kuomba msaada.

Amesema baada ya mkewake kuomba msaada, ndipo majirani wakapiga simu kwa Kamanda wa Sungusungu Buyaga Kazimoto, ambaye naye alichukua walinzi wanne wakampuni ya ulinzi wakiwa na silaha za moto kwenda kumkamata mwanaume huyo ndipo yakatokea mauaji.

Anaeleza kuwa wakati walinzi hao kutoka Kampuni Binafsi ya ulinzi Light Ndovu Security, walipofika nyumbani kwa Jackson Joseph alianza kuwakimbia, ndipo mmoja wa walinzi hao Abdul Chacha alimkimbiza na alipomkamata walianza purukushani akapigwa Risasi ya tumboni na kufariki dunia papo hapo.

Aidha, anafafanua kuwa baada ya tukio hilo la mauaji, kesho yake Mei 18 ndipo Wananchi wa eneo hilo wakashikwa na hasira, wakidai wamechoka kuonewa na viongozi akiwamo Mwenyekiti wa Kitongoji na Kamanda wa Sungusungu, na kuamua kuharibu mali zao ikiwamo kuchoma moto nyumba, pikipiki na kuvunja duka na Ofisi ya kitogonji.


“Jeshi la Polisi tumashikilia mlinzi wa Kampuni ya ulinzi binafsi ya Light Ndovu Securty Abdul Chacha kwa tukio hili la mauaji ya Jacskon Joseph, na upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,”alisema Kyando.

Aidha, alisema pia wanaendelea na upelelezi wa kubaini watu ambao walihamasisha fujo, na kusababisha wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuepelekea uharibifu wa mali, huku akibainisha kuwa mwili wa marehemu wameshakabidhiwa ndugu zake kwa mazishi.

Katika hatua nyingine Kamanda Kyando, alisema Jeshi hilo watafanya ukaguzi wa Makampuni yote ya ulinzi mkoani humo, ili kuona kama walinzi hao wamepitia mafunzo ya kijeshi na kuepuka matumizi holela ya silaha za moto na kusababisha mauaji.

CHANZO:SHINYANGA PRESS

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso