MARAIS WALIOSALITIWA KATIKA NDOA - AFRIKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 24 April 2022

MARAIS WALIOSALITIWA KATIKA NDOA - AFRIKA

 


Na Ally Lityawi,

Ndoa nyingi duniani zimeparanganyika kutokana na usaliti wa mmoja wa mwenza.Upepo mbaya huu katika bahari ya huba umewakumba watu wa kada mbalimbali.

Usaliti huu umebomoa mapenzi ya watu mashuhuri na maarufu duniani,miongoni mwa waliokumbwa na dhoruba hilo la usaliti ni Viongozi wakuu sita barani Afrika,ambao ni hawa wafuatao;

1;MFALME MSWATI III.

Kinara wa wake wengi Duniani katika karne hii,Mfalme Mswati III wa Swaziland,ambaye kutokana na mila na desturi za nchi hiyo zinamruhusu kila mwaka kuoa binti bikira,hakusalimika na upepo wa usaliti katika mapenzi.

King Mswati III inadaiwa kusalitiwa na mmoja wa wake zake aliyefahamika kwa jina la Nothando Dube,ambaye alinaswa akitoa uroda kwa Waziri wa Sheria wa nchi hiyo,Ndumiso Mamba.

Malkia huyo wa Mfalme,alilazimika kutengwa.Hata hivyo alifanikiwa kutoroka katika nchi hiyo na kukimbilia uhamishoini katika nchi ya Afrika Kusini na kuishi  mpweke.

Pamoja na maisha ya upweke aliyodumu nayo hadi mwaka 2019,alipofariki dunia mara kadhaa alikuwa akinukuliwa akimtupia tuhuma Mfalme Mswati III kwa maamuzi aliyochukua ya kumuoa akiwa msichana mdogo wa miaka Kumi na Sita.

Alikuwa akidai katika umri huo aliokuwa nao,akili zake zilikuwa hazijapambanua maana ya mapenzi,hivyo kuolewa pasipo kujua maana ya kupenda.

2;RAIS MANDELA WA AFRIKA YA KUSINI.

Rais wa kwanza wa Afrika Kusini,Nelson Mandela,na mzalendo wa Bara la Afrika,naye katika maisha yake alikumbwa na ombwe  la usaliti kutoka kwa mkewe kipenzi,Winnie Mandela.

Mvumo wa usaliti aliotendwa ulitamalaki dunia nzima,kiasi cha Mwanapainduzi huyo wa Afrika kuamua kutoa Talaka,na Ulimwengu mzima kujiridhisha kuwa Winnie alimsaliti Mandela.

Winnie alishutumiwa kuwa na mahusiano ya kingono na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ustawi wa Jamii wa chama cha ANC,Dali Mpofu,tangu Mandela akiwa gerezani na hata baada ya kuachiwa huru na Makaburu.

3; RAIS MUGABE WA ZIMBABWE.

JONGWEEE ZIMBABWEEE....
Rais Robart Mugabe ama hakika alikuwa Jogoo la Zimbabwe.Nguli huyu wa siasa zenye tija kwa nchi yake,misimamo yake iliyojaa utata haikuwa sababu ya mkewe Grace aliyeonekana kuwa na pepo la ngono kushindwa kumsaliti.

Usaliti wa kwanza uliobainika kutendewa Rais Mugabe,ni pale mkewe alipoamua kugawa tunda kwa aliyekuwa Gavana wa Benki ya nchi ya Zimbabwe,aliyefahamika kwa jina la Gideon Gono.

Gono aliyekuwa rafiki kipenzi wa Rais Mugabe,alipoteana duniani baada ya mwenye mali kutambua utamu wake anaunajisi.Pia kifo kilimpigia hodi na kumuondoa duniani Peter Pamire naye alipobainika analamba asali ya Jongwe Mugabe.

Ni James Makamba pekee aliyebainika kuonja asali ya Rais Mugabe na asikumbane na ghadhabu za mkongwe huyo wa siasa Afrika baada ya kufanikiwa kuitoroka nchi hiyo.


4; JACOB ZUMA WA AFRIKA KUSINI.

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini,Jacob Zuma,naye alikumbana na masahibu haya,baada ya mkewe Nompumeleo Ntuli,kudaiwa kutoa uroda kwa mlinzi wa karibu aliyetambulika kwa jina la Phinda Thomo.

Hata hivyo mlinzi huyo alikutwa amekufa nyumbani kwake mnamo mwaka 2010 na hakuna uchunguzi uliofanyika kuhusiana na kifo chake.


5; RAIS CHILUBA WA ZAMBIA.

Jinamizi hili la Marais kusalitiwa na wake zao pia lilipiga hodi kwa aliyekuwa Rais wa Zambia wakati huo,Frederick Chiluba,ambaye hakuwa na simile zaidi ya kuamua kumtimua Ikulu aliyekuwa mkewe Vera.

Maamuzi hayo ya kumtaliki mkewe aliyachukua mnamo mwaka 1991,baada ya kumshutumu ana mahusiano ya kingono na Mfanyabiashara maarufu nchini humo,aliyejulikana kwa jina la Mactribouy Archie.

6; RAIS EYADEMA WA TOGO.

Rais wa Togo;Gnassigbe Eyadema,ambaye aliiongoza nchi ya Togo miaka ya 1960,alikumbana na dhahama hii baada ya kubaini mkewe kipenzi ana mahusiano ya mapenzi ya ngono na mmoja wa Wakuu wa Mkoa katika utawala wake.

Hapa yatupasa kujiuliza kwanini utokee usaliti? Na yatupasa kufahamu mwanamke akitaka jambo lake liwe linakuwa na tukumbuke kwamba usaliti huu wa mapenzi hauna cheo,umaarufu,utajiri ama umaskini; yeyote humkuta.

Tena ifahamike kwamba usaliti haukuanza karne tuliyopo bali tangu karne na karne na enzi za manabii na mitume Ukisoma vitabu vya Mwenyezi Mungu utakutana na matukio ya usaliti.

Mfano rejea Kisa cha NABII YUSUF kwa kusoma Biblia MWANZO 39;11 - 20, na katika Quran Tukufu soma SURAT YUSUF Aya ya 23 hadi 25.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso