HOUSE GIRL AUAWA, MUUAJI KANYWA SUMU ILI AJIUE AKANUSURIKA PWANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 22 April 2022

HOUSE GIRL AUAWA, MUUAJI KANYWA SUMU ILI AJIUE AKANUSURIKA PWANI


Jeshi la Polisi Mkoani Pwani linamshikilia mtu mtu mmoja mwanaume (27) jina limehifadhiwa kwa tuhuma za mauaji kwa kumshambulia na kitu chenye ncha kali mfanyakazi wa ndani aliyejulikana kwa jina la Dawiya Mshihiri (30).

IMG-20220328-WA0096


Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo kwa waandishi wa Habari ilieleza kuwa mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi wa kulisha mifugo anadaiwa kufanya tukio hilo April 20 majira ya saa saba mchana katika mtaa wa Mkoani B wilaya ya Kibaha

Kamanda Lutumo amesema katika tukio hilo Mtuhumiwa alimshambulia Dawiya kwa kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili na kumsababishia kifo.

Aidha ameeleza kuwa mtuhumuwa baada ya kutekeleza tukio hilo alijaribu kunywa sumu lakini hakufanikiwa, alikamatwa na kupelekwa katika hospitali ya Rufani ya Tumbi kwa ajili ya matibabu akiwa chini ya ulinzi.

Kamanda ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kinaendelea kuchunguzwa pindi uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Kufuatia tukio hilo rai imetolewa kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na endapo kutakuwa na tatizo watoe taarifa kwa mamlaka husika kwa msaada zaidi.

Kamanda Lutumo amesema mtuhumiwa pamoja na marehamu wote walikuwa wafanyakazi katika nyumba ya Samweli.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mkoani B Shabani Kasamia amesema alipata taarifa ya tukio hilo akiwa Mailimoja ndipo alipopiga simu polisi na kuwajulisha.

Aliendelea kueleza kuwa walipofika katika nyumba hiyo wakiwa na polisi walikuta tayari mfanyakazi huyo akiwa ameshafariki akiwa ndani ya nyumba hiyo huku kukiwa na watoto ambao walikua wanashinda na dada huyo.

Alieleza kuwa polisi walipozunguka nyuma ya nyumba kukagua walimkuta kijana huyo akiwa amelala kwenye kitanda nyumba ya uani akiwa amekunywa sumu.

"Polisi walimchukua na kumpeleka katika hospitali ya Rufani ya Tumbi kwa ajili ya matibabu ili aweze kutoa ushirikiano wa tukio hilo."alisema

Kaka wa marehemu Miraji Mshihiri amesema alipata taarifa za kifo cha mdogo wake saa 12 jioni na kwamba marehemu alikuwa msaada mkubwa kwake na msiba huo ni pigo kwa familia.

Majirani wameeleza kuwa wafanyakazi wote wamekuwa wakifanya kazi katika nyumba hiyo kwa muda mrefu na hawakugundua kama kulikua na tatizo baina yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso