MGOMBEA UDIWANI KATA YA NGOGWA ABEL MABAO AREJESHA FOMU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 27 August 2025

MGOMBEA UDIWANI KATA YA NGOGWA ABEL MABAO AREJESHA FOMU






Mgombea udiwani wa Kata ya Ngogwa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Abel Mabao,  agosti 27, 2025 ameweka historia baada ya kurejesha fomu za kugombea nafasi hiyo katika ofisi za kata hiyo.

Mabao, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mabao Investment, amewasili katika ofisi za kata akiwa na wafuasi wake na kupokelewa na mtendaji wa kata Pendo Shirima ambaye amepokea fomu hizo kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu, Mabao ameshukuru wafuasi wake na wananchi wa Ngogwa kwa mshikamano waliomuonesha, akiahidi kampeni zenye maadili na kujikita katika maendeleo ya jamii.

Zoezi la urejeshaji fomu za wagombea udiwani limetamatika leo nchini kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso