WATUNUKIWA CHEREHANI NA MASHINE ATAMIZI KUJIAJIRI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 29 April 2024

WATUNUKIWA CHEREHANI NA MASHINE ATAMIZI KUJIAJIRI



Ubalozi wa China nchini, umetoa cherehani 425 na mashine atamizi ya kutotolea vifaranga 250 vyenye thamani ya Sh milioni 79 kwaajili ya kuendeleza kazi za wanawake wajasiriamali nchini.
Akizungumza april 29,2024 jijini Dar es Salaam, wakati akipokea vifaa hivyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth Gwajima amesema watahakikisha vifaa hivyo vinawafikia walengwa kwa wakati.Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth Gwajima

“Tunashukuru sana kwaaji ya kutoa hizi mashine kwaajili ya wanawake wa Tanzania tukio la leo ni mwendelezo mwema wa mataifa mawili tunathamini msaada huu kwa niaba ya wanawake wote tunawashukuru tutahakikisha umoja na mshikamono huu unaendelea,” ameeleza.

Dk Gwajima amesema anatamani kuona wanawake wa Tanzania wakienda China kuona namna wanawake wa China wanavyofanya kazi ili wajifunze.

“Itafanya wanawake kujifunza na kuwekeza katika viwanda vidogo vya ushonaji na udarizi, msaada huu wa vifaa utaongeza ari ya kuongeza kipato na kuchangia uchumi wa taifa kwani vifaa wanavyo,” amesisitiza Waziri huyo.

Amesema zana ya usawa wa kijinsia ni kuongeza nguvu ya wanawake katika ngazi za maamuzi ya maendeleo na sera.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini, Chen Mingjian amesema wanafurahi kuona ushirikiano unazaa matunda ambapo pia walitoa mbegu za soya kwa wakulima wa mkoa wa Ruvuma na wamevuna hivyo kipato cha familia kimeongezeka.

“Tumeshirikiana na taasisi isiyo ya serikali kutoa vifaa vya taulo za kike kwaajili wa kusaidia wasichana na wanawake na hili limekuwa na mafanikio na tangu nimekuja Tanzania nimeona Rais Samia amekuwa anawapa nafasi kubwa wanawake katika maendeleo.

Amesema wanawake wa Tanzania wanafanya jitihada kubwa ya kuendelea kukuza nchi yao nzuri na serikali ya China na Tanzania wanaunga mkono kufanya maisha marahisi ya utendaji kazi kwa wananchi.



Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mary Chatanda amewashukuru China kwa kujali maendeleo ya wanawake na kuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano wakati wote.

“Tuna mahusiano mazuri na chama tawala cha China napenda kushukuru ubalozi wa China kwa zawadi hii kwani kufikia 50 kwa 50 ni uchumi imara wenzetu wa China kwa kupitia China women fedaration wamefanikiwa tayari.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso