WANANCHI WA MTAA WA NYASHIMBI WASISITIZWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KA TIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 26 November 2024

WANANCHI WA MTAA WA NYASHIMBI WASISITIZWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KA TIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA.


NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA


Wananchi wa Mtaa wa Nyashimbi, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, wamehimizwa kudumisha amani na utulivu katika kipindi chote cha uchaguzi utakaofanyika kesho, Novemba 27, 2024, wakati wa zoezi la kupiga kura.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Kahama, Simbila, amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kupiga kura na kurudi nyumbani bila kufanya vurugu yoyote, akionya kwamba serikali imejipanga kuhakikisha usalama katika maeneo yote ya kupigia kura.


Simbila ameongeza kuwa amani ya Tanzania ni muhimu na kwamba kila mtu ana wajibu wa kulinda amani hiyo ili kudumisha maendeleo pia Amtoa wito kwa wananchi kuwahi vituoni kwani zoezi la kupiga kura litaanza mapema saa mbili asubuhi.


Mwananchi Mwajuma Mrisho amesisitiza kuwa viongozi watakaochaguliwa kesho wanapaswa kutekeleza ahadi zao na kushirikiana na wananchi katika masuala ya maendeleo kama vile miundombinu ya barabara, maji, umeme, elimu, na afya.


Rose Stephano, kwa upande wake, alitoa wito kwa viongozi kuwa waaminifu na wenye hofu ya Mungu katika kutekeleza majukumu yao.


Gerald Embaga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura, akisisitiza kuwa ni haki yao ya msingi, Aidha amewataka viongozi wapya kuboresha huduma mbalimbali katika mtaa wa Nyashimbi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso