BINTI WA MIAKA 16 AJERUHIWA KWA RISASI MKOANI MARA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 5 March 2024

BINTI WA MIAKA 16 AJERUHIWA KWA RISASI MKOANI MARA

Neema Omari (16), mkazi wa Kijiji cha Kewanja Wilaya ya Tarime mkoani Mara amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mkoani Mara, akidaiwa kupigwa risasi miguuni na polisi.


Picha hii haina uhusiano na iliyotumika eneo la tukio



Neema alifikishwa hospitalini hapo Machi 2, 2024 baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Nyamwaga wilayani Tarime alikopelekwa akitokea katika Kituo cha Afya cha Nyamongo alikopelekwa kwa matibabu baada ya kujeruhiwa.


Akizungumza hospitalini hapo Machi 4, 2024, daktari wa kitengo cha mifupa, Elias Nguti amesema baada ya kumfanyia uchunguzi wa awali ilibainika binti huyo ana vipande vya chuma kwenye miguu yote miwili.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Tarime/Rorya, Mark Njera alipotafutwa azungumzie tukio hilo, simu yake haikupokewa na alipotumiwa ujumbe wa maneno, amejibu kwa ufupi, “niko kikaoni nitatoa taarifa kwenu juu ya tukio hili."


Soma kwa undani www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso