AJIUA CHANZO DENI ANALODAIWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 22 August 2023

AJIUA CHANZO DENI ANALODAIWA


Mwanaume wa miaka 40, mkazi wa Kijiji cha Manyata katika Kaunti ya Murang’a, anadaiwa kujitoa uhai kukwepa deni la Sh30, 000 (sawa na Sh520, 000 za Tanzania) ambalo linadaiwa kuwa rushwa kwa polisi wa Kituo cha Sabasaba.Kwa mujibu wa msemaji wa kamati ya marafiki kuhusu maziko ya ndugu huyo aliyejulikana na kwa jina la Joseph Murigi, imeelezwa kuwa polisi hao walikuwa wakimdai hongo, ili wasimshtaki kwa hatia ya kupiga picha za ‘aibu’ mitandaoni.


“Murigi alikuwa na kashfa fulani kutoka kwa mpenzi wake. Picha za aibu za mpenzi huyo zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii na akaorodheshwa kama mshukiwa mkuu,” amesema James Guchu ambaye ni msemaji wa kamati hiyo.


Guchu aliongeza kuwa, baada ya mwanamke huyo kuripoti katika kituo cha polisi cha Sabasaba, Murigi alianza kutafutwa ili atiwe mbaroni.


“Polisi walifanikiwa kumkamata na kumfikisha kituoni kwao hapo Sabasaba, ambapo kesi iliandaliwa kienyeji na hivyo kukutwa na hatia. Aliamriwa kulipa faini ya Sh30, 000; ambazo zilikuwa zikabidhiwe kwa mkuu wa kituo,” amesema.


Kwa kuwa marehemu hakuwa na pesa hizo, inadaiwa kwamba baadhi ya marafiki na familia kwa pamoja tulichangishana fedha ya haraka na kufanikiwa kupata Sh15, 000.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso