WANAFUNZI WATATU WASIOONA WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA MOTO,RC MJEMA AWATAKA MATRON WAWE WANALALA NDANI,SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 24 November 2022

WANAFUNZI WATATU WASIOONA WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA MOTO,RC MJEMA AWATAKA MATRON WAWE WANALALA NDANI,SHINYANGA

Mkuu wa mkoa shinyanga,Sophia Mjema amewataka viongozi katika shule za mabweni zilizopo mkoani humo kuimarisha uangalizi na usimamizi wa watoto kwa kuongeza wasimamizi (Matron,Patron) ili kuimarisha usalama wa watoto wawapo katika mabweni yao.NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Maagizo hayo ameyatoa leo,Novemba 24,2022 akiwa anatoa pole katika kituo cha kulea watoto wenye uhitaji maalum(viziwi,albino,na vipofu) Buhangija kilichopo Manispaa na Mkoa Shinyanga kufuatia vifo vya watoto watatu,vilivyosababishwa na kuungua kwa bweni la kulala watoto hao.


Mjema,ametoa maagizo hayo kwa kufuatiwa na matukio ya ajali za moto yanayotokea katika shule za bweni huku akisikitishwa na vifo vya watoto hao Nilium Limbu,Caleen Mayenga na Catherine Paulo,waliopoteza maisha baada ya kuungua kwa bweni B katika shule hiyo huku akitoa pole kwa wazazi na walezi pamoja na kuwataka wawe na subra katika kipindi hichi cha majonzi.


Aidha Mjema amelitaka Jeshi la zimamoto Mkoani Shinyanga,waanzishe utaratibu wa kutoa elimu katika Shule zote jinsi ya kutoa huduma ya kwanza linapotokea janga la moto ili kuondokana na adha ya kupoteza mali na maisha kwa wanafunzi katika shule hiyo.


“Nimepata taarifa nikiwa safarini Mwanza katika kikao na Makamu wa Raisi Philipo ambapo anatoa pole kwa wanashinyanga wote, nitoe maagizo kwa walimu na uongozi kwa ujumla wa shule,muweze kuongeza wasimamizi wa wanafunzi(Matron,Patron),kwa kila chumba,na wawe wanalala vyumbani (ndani) na siyo nje”Amesema Mjema.


Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa Shinyanga,ACP Janeth Magomi,amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa moto huo ili kubainisha chanzo chake ambacho kimesababisha vifo vya watoto watatu Nilium Limbu (12)mwanafunzi wa darasa la kwanza,Caren Mayenga(10) mwanafunzi wa darasa la kwanza, na Catherine Paulo(10) mwanafunzi darasa la pili,wote ni wasioona ambapo Bweni hilo lilikuwa na wanafunzi 32(Wasioona 11,viziwi 3 na albino 18).


Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija,Fatuma Gilalah,Ameeleza juhudi alizozifanya Msimamizi wa wanafunzi hao ambaye alitoa taarifa ili kupatiwa msaada na kuweza kufanya uokozi kwa wanafunzi na mali zilizokuwa katika Bweni hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso