MTOTO ANUSURIKA NA KIFO KWA KUSHAMBULIWA NA CHATU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 26 November 2022

MTOTO ANUSURIKA NA KIFO KWA KUSHAMBULIWA NA CHATU

Mvulana mwenye umri wa miaka mitano raia wa Australia amenusurika kifo baada ya kuumwa na chatu ambaye ppia alimburuta hadi kwenye bwawa la kuogelea.


Chatu huyo alikua na ukubwa wa takriban mara tatu ya umbo la kijana huyo.


Kwa mujibu wa baba yake mzazi Kijana Beau Blake alikuwa akifurahia kuogelea nyumbani kwao wakati chatu huyo mwenye urefu wa mita 3 sawa na futi 10 alipomvamia.


Lakini Beau yuko katika hali nzuri na kwamba anaendelea vyema ingawa ana majeraha madogo tu.


Tukio hilo limeendelea kuzungumziwa katika eneo analoishi kijana huyo.

CHANZO: EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso