JAMBAZI LAUAWA NA POLISI KILIMANJARO WAKATI LIKIJARIBU KUPORA PIKIPIKI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 28 October 2022

JAMBAZI LAUAWA NA POLISI KILIMANJARO WAKATI LIKIJARIBU KUPORA PIKIPIKI

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kumuua mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka 30 na 35 aliyekuwa anajihusisha na matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha ambapo Oktoba 26 majira ya saa mbili usiku alifanya jaribio la kupora pikipiki.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema jambazi huyo alikamatwa na pisto aina ya Broin yenye namba A 920 580 ikiwa na risasi 9.


Kamanda Maigwa amesema uchunguzi wa awali umebaini silaha hiyo inamilikiwa na mtu ambae jina limehifadhiwa na iliibiwa kwa mmiliki huyo ambae ni mkazi wa Manyara.


Jambazi huyo alikamatwa pia na silaha aina ya Sime ambapo mtuhumiwa alifariki wakati akipelekwa Hospitalini na mwili wake umehifadhiwa katika hiospital ya kanda ya KCMC Moshi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso