WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA NA POLISI WAFANYA MDAHALO KUJADILI MASUALA YA ULINZI NA USALAMA KWA WANAHABARI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 4 August 2022

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA NA POLISI WAFANYA MDAHALO KUJADILI MASUALA YA ULINZI NA USALAMA KWA WANAHABARI

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) kwa Ufadhili wa International Media Support (IMS) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi  Mkoa wa Shinyanga limehamasisha waandishi wa habari kuwa wanafika kwenye eneo la tukio ili kupata habari na taarifa za kutosha kuhusu kilichotokea.



Rai hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) kwa Ufadhili wa International Media Support (IMS) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).



“Waandishi wa habari fikeni eneo la tukio, jitahidini kufika kwenye matukio ili mpate taarifa kwa kina lakini pia ni vyema mkawa mnapeana taarifa kwa sababu kila chombo cha habari kina wateja wake “,amesema Nyandahu.



Aidha amesema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na waandishi wa habari huku akiomba kuwe na mahusiano mazuri ya kiutendaji ili kuondoa migongano mbalimbali ili kuboresha mahusiano zaidi na kuimarisha ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari.



"Mnapoandika habari za masuala ya ukatili mzifanyie mwendelezo, mnapoandika habari zenu msiishie njiani andikeni matokeo ya kesi mahakamani ili jamii ijifunze na kuachana na matukio ya ukatili wa kijinsia", Afande Analyse Kaika kutoka Dawati la Jinsia.



Akiwasilisha mada kuhusu usalama wa waandishi wa habari, Mwandishi wa Habari Mkongwe, Paul Mabuga amesema mahusiano ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari yanategemeana hivyo ni vyema wakafanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana.



Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SPC, Greyson Kakuru amesema waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wapo tayari kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi huku akiwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23,2022.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) Greyson Kakuru akisoma hotuba leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).

Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga, Jeremiah Zitta akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) 

Mwandishi wa Habari Mkongwe, Paul Mabuga akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) 
Mwandishi wa Habari Mkongwe, Paul Mabuga akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) 
Mwandishi wa Habari/Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) 

Picha ya pamoja wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso