PUNDA WASABABISHA MTOTO KUJIUA KWA KUNYWA SUMU-NJOMBE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 4 August 2022

PUNDA WASABABISHA MTOTO KUJIUA KWA KUNYWA SUMU-NJOMBE



Mtoto mmoja wilayani Makete mkoani Njombe amekutwa amefariki kwa kunywa sumu sababu ikielezwa kukalipiwa na Baba yake aliemuonya kwa kuwatelekeza Punda walioingia shambani na kula mazao ya mtu.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Njombe, Hamis Issah amesema mtoto huyo aliwaacha Punda na kwenda kucheza na watoto wenzake na baada ya Punda hao kulipotiwa na mwenye shamba kuwa wamekula mazao yake baba wa mtoto huyo alimuonya mtoto wake na hivyo mtoto kuchukua uamuzi huo.


Hata hivyo kamanda Issah amewataka wazazi na walezi kubuni njia bora ya kuwaonya watoto kipindi hiki cha likizo huku akiwataka watoto kuzingatia maadili ya wazazi wanayowapa ili kujenga jamii bora.


Amesema watoto wa sasa sio kama wa zamani hivyo inapaswa wazazi kuwa waangalifu katika kitendo cha kuwaonya.

chanzo:Millardayo tv

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso