

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 7 majira ya saa nane mchana katika maeneo ya Mama John jijini Mbeya alipokuwa akiendelea kuwatapeli watu.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amelishukuru Jeshi la Polisi kitengo cha IT kwa jitihada za kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akitumia akaunti yake kuwatapeli watu.
Aidha Homera amewasihi viongozi wenzake wakiwamo wanasiasa kujenga utamaduni wa kukagua mitandao yao ya kijamii.
Mtuhumiwa huyo Warren Mwinuka amekiri kufanya kitendo hicho
CHANZO EATV
No comments:
Post a Comment