MBUNGE ALIYETEKWA MWILI WAKE WAPATIKANA AKIWA AMEKATWA KICHWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 23 June 2022

MBUNGE ALIYETEKWA MWILI WAKE WAPATIKANA AKIWA AMEKATWA KICHWA


Watu wenye silaha kusini mashariki mwa Nigeria wamemuua kwa kumkata kichwa mwanasiasa mwingine katika jimbo la Anambra.


Msemaji wa polisi, Ikenga Torchukwu amesema kuwa mwili wa Nelson Achukwu-mbunge wa zamani katika jimbo la Anambra ulipatikana Jumanne baada ya kutekwa nyumbani kwake mapema mwezi huu.


Haijabainika ni nani aliyetekeleza utekaji nyara na mauaji ya mwanasiasa huyo mlemavu na Ripoti zinaonyesha ilikuwa ni mara ya pili yeye kutekwa nyara katika miezi kadhaa na pesa ililipwa ili kuachiliwa wakati wa kutekwa nyara mara ya kwanza.


Mamlaka mara nyingi zimewalaumu watu wanaotaka kujitenga wanaodai jimbo lililojitenga la Biafra kwa ghasia zinazozidi kuwa mbaya kusini mashariki mwa Nigeria.


Hivi karibuni mbunge wa eneo hilo na msaidizi wake pamoja na afisa wa kijeshi na mwenza wake wa kike pia walikatwa kichwa na hivi karibuni Nigeria inakabiliana na ghasia zisizokwisha zinazofanywa na makundi mbalimbali yenye silaha kote nchini humo.

Chanzo:BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso