TANZANIA YAZINDUA KAMPENI YA MGOMBEA WA NAFASI YA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI KANDA YA AFRIKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 9 May 2024

TANZANIA YAZINDUA KAMPENI YA MGOMBEA WA NAFASI YA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI KANDA YA AFRIKA

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemtangaza Mgombea wa Nafasi ya Mkurugenzi wa Afrika katika Shirika la Afya Duniani (WHO)  Dkt. Faustine Ndugulile ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Tanzania wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  January Makamba (Mb.)


Akitambulisha sifa na uwezo binafsi wa mgombea huyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  January Makamba (Mb.) amesema kuwa  Ngugulile ni mgombea sahihi mwenye uwezo wa kazi na kufanya mageuzi na maboresho katika ya Sekta ya Afya.


Aidha, ameeleza kuwa Ndugulile alipokuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Afya aliweka kipaumbele cha kusimamia suala la kutunga, kusimamia sera na kuratibu mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha usimamizi wa sekta ya afya nchini unaimarika kwa ajili ya kujenga nguvu kazi imara ya Taifa.


“Kupatikana kwa nafasi hii kutaiwezesha Tanzania kuimarika zaidi katika utekelezaji wa Diplomasia ya Afya ambayo ni muhimu katika Diplomasia yetu kwa ujumla hususan katika usimamizi wa mipango, maarifa na rasilimali ulimwenguni.’’ Amesema  Waziri Makamba


Dkt. Faustine Ndugulile  ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Tanzania wa Jimbo la Kigamboni jijini   Dar-es-Salaam

 

Mbali na hayo Waziri Makamba ameeleza kuwa kufauatia  jitihada mbalimbali za kidiplomasia zilizofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki tayari mgombea wa Tanzania ameungwa mkono na Nchi 16 Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi zingine 7 kutoka Afrika, hivyo kuipa Tanzania mtaji wa jumla ya kula 23 katika kinyang’anyiro cha kuwania nafaisi hiyo.


Naye Waziri wa Afya, Ummy  Mwalimu amemwelezea   mgombea  Dkt. Ndugulile  kuwa akiwa Naibu Waziri katika Wizara ya Afya alifanya jitihada katika kuimarisha afya ya msingi kwa kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kutoka Serikalini na wadau wa maendeleo.


Waziri  Ummy  Ameongeza kuwa Ndugulile ametoa mchango mkubwa kwenye usimamizi wa maboresho  ya  afya ya mama na mtoto na lishe na chanjo ambapo usimamizi huo umewezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya wajawazito na watoto.

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso