WANANCHI KISHAPU WAOMBEA AMANI YA TANZANIA MIAKA 60 YA MUUNGANO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 22 April 2024

WANANCHI KISHAPU WAOMBEA AMANI YA TANZANIA MIAKA 60 YA MUUNGANO



Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Mkude amewasihi wananchi kuendeleza desturi ya kuliombea taifa la Tanzania lidumu na amani,umoja na mshikamano kwa maslahi mapana ya maendeleo.

Dc Mkude ameyasema hayo leo April 22,2024 alipokuwa kweye maombi na dua maalumu ya kuliombea taifa kufuatia maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano maombi yaliyokutanisha viongozi na wananchi wa madhehebu yote yaliyofanyika katika viwanja vya SHIRECU wilayani humo.


"Watanzania wenzangu kipekee nimshukuru Mungu kwa upendo na huruma zake kutupa uzima na kuishi kwenye taifa letu zuri la Tanzania, zaidi sana neema ya kumjua na kutambua amani,umoja mshikamano vinapatikana kwake ndio maana siku hii tumeacha vyote na kuja kumuomba Mungu kwa pamoja katika viwanja hivi ili aendelee kulitunza taifa na viongozi wetu" ,amesema Mkude.


Sanjari na hayo amewasihi vijana pamoja na wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa kuepukana na siasa na maneno ya uchochezi yatakayopelekea kupoteza amani,umoja,upendo na mshikamano kwa wananchi.


Kwa upande wake mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kishapu Jiyenze Seleli amesema Chama Cha Mapinduzi ambacho ni chama tawala wanaheshimu maamuzi ya wananchi ikiwa wamepewa dhamana ya kuongoza nchi hivyo wanaendelea kuhakikisha amani naumoja ulioanzishwa na waasisi Mwalimu Julias Nyerere wa Tanganyika na Sheikh Abeid Amani Karume wa Zanzibar unaendelea na hawako tayari kuona unavurugika kwa utashi wa baadhi ya watu wenye nia ovu.


Hata hivyo sheikh wa tarafa ya Kishapu Adam Njiku aliyemwakilisha sheikh wa wilaya hiyo amesema Mwenyezi Mungu pekee ndiye awezaye kutoa ulinzi licha ya Jeshi kuwepo na viongozi kwa sababu anajua na kitambua moyo wa kila mwanadamu.

Baadhi ya Viongozi kutoka madhehebu ya kikristo na kiisilamu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye viwanja vya shirecu leo wilayani humo kuliombea taifa la Tanzani amani na umoja kuelekea miaka 60 ya muungano.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso