NMB KARIBU YAKO HAACHWI MTU NYUMA YATIKISA SHINYANGA,WANANCHI TINDE WACHANGAMKIA NMB PESA AKAUNTI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 10 April 2024

NMB KARIBU YAKO HAACHWI MTU NYUMA YATIKISA SHINYANGA,WANANCHI TINDE WACHANGAMKIA NMB PESA AKAUNTI



 
Mamia ya Wakazi wa wilaya ya Shinyanga na Mkoa wa Shinyanga wamefurika huduma ya NMB Pesa Akaunti pamoja na huduma ya Faraja Bima katika kampeni ya Kuhamasisha Ufunguaji wa Akaunti ya NMB Pesa Akaunti Isiyo na Makato ya Mwezi inayotolewa na Benki ya NMB pamoja na Akaunti ya Faraja Bima.


Kampeni hiyo inayoendeshwa na Uongozi wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi ,NMB Tawi la Manonga kwa kushirikiana na Amos John (Mc Mzungu mweusi ) wameendesha kampeni ya "NMB Karibu yako haachwi mtu nyuma" iliyofanyika leo katika mnada wa Tinde wilaya ya Shinyanga kwa kuwapa nafasi wananchi waliojitokeza katika mnada huo kufungua Akaunti za Shilingi 1,000/= Tu na Chapu Chapu Akaunti zoezi lililoenda sambamba na kuelezea faida za kuwa na bima ya faraja.


Akielezea lengo la kutembelea mnada wa Tinde Afisa Masoko wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Albin Mpona amesema kuwa Benki ya NMB ambayo inafanya kazi kubwa kwa ajili ya ustawi wa maisha ya watanzania kwa kuanzisha NMB Pesa akaunti , ambayo kwa shilingi 1,000/= akaunti ambayo itakuwezesha kupata huduma zote za kifedha, ikiwemo mikopo, kutuma, kupokea, kutoa fedha na kulipia bili mbalimbali.


“Sasa, mimi niwaombe kitu kimoja Wana Tnde sisi tupo wengi sana na ‘buku buku’ zipo nyingi sana miongoni mwenu, changamkieni fursa kwa kufungua akaunti za NMB Pesa ili mujiwekee akiba, lakini mpate kunufaika na huduma za kifedha za benki hii", amesema Mpona.


Awali, afisa Masoko wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Albin Mpona amewahakikishia Wana Tinde na Watanzania kwa ujumla, kwamba NMB imewaletea fursa inayoenda kubadili maisha yao, kupitia NMB Pesa Akaunti, ambayo ni ya kidigitali unayofunguliwa kwa Shilingi 1,000 tu, ikiwafikia ikiwa na fursa nyingi.


"Fursa ya kwanza inayokuja na akaunti hii ni kuwa unaingia moja kwa moja kwenye Huduma Jumuishi za Kifedha kupitia NMB, watoa huduma wametapakaa kote kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa sehemu ya huduma hii inayokuja chini ya kaulimbiu ya ‘Haachwi Mtu".


"Kupitia NMB Pesa, utakuwa umeingia moja kwa moja katika huduma ya NMB Mkononi, inayokupa wigo mpana wa kujihudumia na kuhudumiwa kibenki bila kuja matawini ama katika ofisi za benki yetu ambako utafanya miamala na malipo na manunuzi kidigitali".


"Pia, rekodi zako kipesa kupitia NMB Pesa Akaunti, zitakuongezea fursa, kwani kubwa kuliko yote utaweza kukopa hadi shilingi 500,000 kupitia Mshiko Fasta, huduma ya mikopo isiyohitaji dhamana yoyote wala kujaza fomu. Hapo vipi, haujabadilisha maisha yako?", amesema Albin Mpona

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso