MALECELA ATAMANI SERIKALI MOJA YA MUUNGANO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 16 April 2024

MALECELA ATAMANI SERIKALI MOJA YA MUUNGANO



Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, Dk. John Malecela amesema anatamani kuona ndoto ya kuwa na Serikali Moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafikiwa.



Dk. Malecela ameyasema hayo jana Aprili 15 Jijini Dodoma nyumbani kwake wakati wa mahujiano maalum na Habari Leo Digital kuelekea sherehe za maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 Jijini Dar Es Salaam.

“Sisi tulikuwa na nia ya Muungano kutoka Serikali Mbili kwenda Serikali Moja. Tumejitahidi mpaka tumefika hapa. Matumaini yangu, vijana ambao ndio Taifa la leo mtajitahidi kwenda huku tulipotaka kufika lakini hatukufika kutoka Serikali Mbili kwenda kuwa na Serikali Moja,” amesema Dk. Malecela.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso